Badirisha ku Medicaid na CHIP: Guide ya Batu ba Mupya

Tengenezeshwa:10/1/2026
Mnamo tarehe 1 Octobre 2026, kanuni za ufadhili ya serikali kuu kwa ajili ya Medicaid na Mpango ya Bima ya Afya kwa Batoto (CHIP) zilibadilika. Mabadiliko iyi inaweza kuathiri baadhi ya batu ba mupya nchini Marekan. Soma makala hii ili kujifunza zaidi.
Image
a stethoscope on a desk with a government building in the background

Mnamo tarehe 1 Octobre 2026, kanuni za ufadhili ya serikali kuu kwa ajili ya Medicaid na Mpango ya Bima ya Afya kwa Batoto (CHIP) zilibadilika. Mabadiliko iyi inaweza kuathiri baadhi ya batu ba mupya nchini Marekan Unaweza kupokea information rasmi inayosema kuwa bima yako ya afya itabadilika au kuisha. 

Unaweza kuwa na chaguzi tena za bima za afya au huduma ya afya ya gharama kidogo. Lakini chaguzi zako ina endana na hali yako ya uhamiaji, kipato, age, ujauzito, bukubwa ya famille, na jimbo unaishi ndani. Guide iyi ya "Settle In" unaeleza mambo enye ilibadilika, ni bima nyingine au huduma za afya za gharama kidogo zipi zinazoweza kupatikana, na nini unaweza kufanya sasa. 

Muhimu: Usi stop bima yako ya sasa ya afya kwa sababu ya article iyi. Ngoya information rasmi kutoka kwa mpango wa Medicaid au CHIP ya jimbo lako. Kama huelewi information hiyo, mwombe mtaalamu unayemwamini anayesaidia mambo ya bima ya afya au mtoa huduma wa mambo ya makazi yamupya aipitie pamoja nawe. Kanuni hutofautiana kufatana na jimbo na hali za mtu yepeke. 

Nini njo Medicaid na CHIP? 

  • Medicaid ni mpango wa serikali inaotoa huduma ya afya ya bure au ya gharama kidogo kwa watu wanaostahiki na wenye kipato ya chini  
  • CHIP ni mpango ya serikali ambao inatoa huduma ya afya bila malipo au gharama kidogo kwa batoto wanaostahiki, na katika baadhi ya majimbo, wajawazito. 

Nini njo ina badirika? 

Kuanzia tarehe 1 Octobre, 2026, ufadhili wa serikali kuu kwa ajili ya huduma kamili za Medicaid na CHIP itahusu makundi machache zaidi ya wahamiaji. Mabadiliko iyi inaweza kuathiri baadhi ya bakimbizi, batu benye baliopata hifadhi, ba survivant ba biashara ya binadamu, na batu benye balioruhusiwa kuingia nchini kwa sababu za kibinadamu, miongoni mwa wengine. 

 

Uhangalishi wa eligibiliter 

Categorie ya uamiyaji Nini njo inaweza kutokea kwa huduma za Medicaid au CHIP zinazofadhiliwa na serikali ya shirikisho baada ya tarehe 1 Octobre, 2026 
Wakazi wa kudumu halali (wenye kadi ya kijani), iwapo wanatimiza kanuni nyingine za mpango huo Inawezekana ubakiye eligible 
Benye banaingia kutoka Cuba na Haiti, ikiwa banatimiza kanuni zingine za mpango huo Inawezekana ubakiye eligible 
Wahamiaji Maalum kutoka Iraqi na Afghanistan, iwapo wanatimiza kanuni nyingine za mpango huo Wanaweza kuendelea kuwa eligible kama wakazi wa kudumu halali au kupitia kundi ya qualification ingine. 
Bakimbizi, batu benye baliopata hifadhi, manusura fulani wa biashara ya binadamu, baadhi ya batu benye balioruhusiwa kuingia nchini kwa sababu za kibinadamu, na bageni bengine fulani ambao habana qualification ingine ya status. Inawezekana auko tena qualifier kupata huduma kamili ya Medicaid au CHIP inayofadhiliwa na serikali ya shirikisho. 

 

Iyi tableau ni guide generalwe tu. Watoto na watu wajawazito bado wanaweza kuwa qualifier katika majimbo yanayotumia chaguo maalum chini ya Kifungu cha 214 cha Sheria ya reauthoriser bupya Mpango wa Bima ya Afya ya Watoto (inayojulikana kama CHIPRA 214). Majimbo mingi pia hulipia programe zabo za afya. Shirika la Medicaid au CHIP la jimbo yako lazima ilipitie upya kesi yako mbele ya kubadilisha huduma yako ya bima. 

Kama utakuya kuwa mkaaji wa kudumu halali baadaye, mulombe mtaalamu wa masuala ya eligibiliter a verifier upya uhalali yako ya kupata mafao hayo. Bahamiaji ba mingi banaweza endelea kusamehewa muda wa kawaida wa kusubiri wa miaka mitano juu bapata huduma kamili za Medicaid au CHIP iwapo baadaye watakuwa wakazi wa kudumu halali. Group zingine zina weza kuwa qualifier kwa ajili ya msamaha. 

Ni fanye nini sasa? 

  1. Fungula kila baruwa ya kutoka Medicaid, CHIP, au mpango yako ya bima ya afya. Tafuta tarehe ya mwisho au maombi ya ma documents. 
  2. Hakikisha kuwa agent wa Medicaid au CHIP wa jimbo lako ana address yako ya sasa, namba ya simu, na email.  Kama una toka, metre a jours ma information pale pale 
  3. Tuma ma document enye banalomba mu wakati yao. Chunga copie wala photo ya kila document enye uli pana. 
  4. Lomba musahanda. Ongeya na mtoa huduma wako ya mpango ya makazi yamupya, msimamizi wa kesi yako, ofisi ya Medicaid au CHIP ya jimbo, au mshauri wa bima ya afya juu upate mwongozo. 
  5. Usi puuziye information yote ya kumaliza bima. Ongeya na agent wa Medicaid au CHIP wa jimbo lako juu kufahamu sababu ya kukatishwa kwa huduma yako ya bima, wakati ambayo isha, na ikiwa unaweza kukata recour kuusu uamuzi huo. 
  6. Panaga kuusu matibabu na matunzo enye inaendeleya. Kama unatumikisha dawa mara kwa mara au unahitaji huduma yakuendeleya, ongeya na mtoa huduma wako wa afya mbele ya mabadiliko katika bima yako juu muongeleye kuusu huduma unazoweza kuhitaji, na ikiwa unaweza kupata dawa za siku 90, na jinsi ya kuendelea kupata huduma baada ya hapo. 
  7. Tafuta matunzo ya bure ama ya bayi kidogo. Tafuta kituo cha afya cha karibu y ya centre communauteur kutumikisha zana ya HRSA ya kutafuta kituo cha afya ama  tafuta Clinique ya bure au ya hisani kwa kutumia zana ya National Association of Free & Charitable Clinics ya kutafuta kliniki.
  8. Lomba mpango ingine ya bima ya afya kabla ya bima yako ya sasa kumalizika muda wake. Kupoteza Medicaid au CHIP inaweza kukuwezesha kujiunga na mpango wa Soko la Bima ya Afya (bima ya afya ya kipekee inayopatikana kupitia HealthCare.gov au tovuti ya Soko la Bima ya Afya ya jimbo lako) au mpango ingine ya bima ya afya inje ya kipindi cha kawaida ya kujiunga. Tuma maombi haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha unaendelea kuwa na bima. 
  9. Angaliya aplication yoyote ya uamiaji enye ina simama. Kama umeomba 'green card', au unaweza kuwa na sifa za kuomba, wasiliana na avocat wako au mtoa huduma za kisheria ili kuongeya kuhusu kumalizika kwa bima yako ya afya.
Je, makala hii ilikusaidia?
0
0