Kazi ya Pamoja
Msaada waki serkali
Shirika ya kiserkali ya kazi za ujamii zinatowa msaada kwa watu wa shirika. Inasaidiya watu wanao kuwa na haja binafsi, kama vile jamaa inayo kuwa na mushahara mudogo, wanao kosa makao, na watu wanao ishi na ulemavu. Mpango was serkali unakuwa ma muda ambao umewekewa mpaka na muelekezo kea wauzuriyaji.
Hizi ni moja wapo ya mipango ya serikali kwaku saidiya wageni:
Mpango ya msaada waki pesa
Kwa watu walio na shida za kupata kazi, mipango miwili yana towa msaada waki pesa kwa muda mfupi: Msaada kwa muda kwa itaji za jamaa (TANF) kwa wazazi wanao Kuwa na watoto na msaada waki pesa kwa wakimbizi (RCA) kwa wale hawajaolewa na wakimbizi ambao wameolewa na hawana watoto.
Mpango wa msaada wa ziada kwa malisho (SNAP)
Mpango wa Usaidizi wa Lishe ya Ziada (SNAP) husaidia watu binafsi na famille za kipato cha chini nchini wa Etats Unis kununua chakula. Washiriki hupokea kadi ya malipo ili kununua kiasi fulani cha chakula kila mwezi. Kiasi cha usaidizi kinatofautiana kulingana na hali na inategemea ukubwa wa familia na mapato. Wageni wanaweza kutuma maombi ya usaidizi wa chakula katika ofisi ya serikali ya mtaa.
Informartion ya sasa: Kwa sababu ya mabadiliko ya hivi majuzi, ustahiki wa SNAP umezuiwa kwa baadhi ya wageni. Wa Refigies, Wakimbizi, walioachiliwa kwa msamaha wa kibinadamu, na watu wengine walio na ulinzi wa kibinadamu ambao hawajazoea hali halali ya ukaaji wa kudumu (LPR) hawastahiki tena manufaa ya SNAP. Paka ba Americain, LPRs, na waingiaji wa Cuba na Haiti pekee ndio wanaosalia kustahiki.
Usalama wa Ziada (SSI)
Hii ni mpango wa jimbo ya msaada waki pesa kwa watu ambao ni walemavu na wa zaidi ya miaka 65 na wanao kuwa na pato ndogo.
Mpango wa msaada kwa watoto
Shirika zimoja hutowa kwa bure ao kwa malipo kidogo kazi zaku chunga watoto kwa watu wenye pato ndogo ili wapate ku tumika ao ku tafuta kazi.
Kazi za Umma
Kila shirika ina kazi za uma zinazo patikana na kila mtu katika shirika. Zifuatazo ni chache ya zile kazi za umma za kawaida.
Msaada waki serkali
Zifuatazo ni chache ya zile kazi za umma za kawaida:
Pango na mapumziko
Pango za jimbo zinakuwa na uwanja wa matembezi na viwanja vya michezo kwa umma. Pango nyingi huwa na kanuni kuhusu nini wageni wana pasha na hawapashwe ku fanya. Pango nyingi za jimbo ni bure, lakini pango zataifa zina weza lipisha pesa ya kuhorozeshwa.
Msaada usio kuwa waki serikali
Shirika fulani za huduma zinaji shugulisha na mikopo kutoka kwa raia binafsi au na jumla ya mikopo na pesa za serikali. Wanakuwa na kundi ya waongozi wanaosimamiya kazi yao na wanatakiwa ku towa ripoti ya umma kwa kila mwaka kuhusu kazi zao, lakini zina tenganishwa na serkali.
Aina hizi zote za shirika kwa ujumla zina kuwa chini ya moja ya ayo makundi matatu ya fwatayo:
Mashirika isiyo ya Kiserikali (NGOs)
Mashirika isiyo ya Kiserikali zina towa kazi kwa eneo zote nchini, kwa kawaida iliyoandaliwa na ofisi ya makao makuu katika muji mkubwa. Zimoja zina weza kutowa hizo msaada kwa wageni. Kiasi, gharama na aina za kazi hizi pishana kutoka mahali kwa mahali, lakini wengi wanatowa zifuatazo:
- Ushauri
- Msaada wa hali yaku hama
- Madarasa ya Kiingereza
- Huduma za ajira
- Kazi za utafsiri
Shirika za jamii (CBOs)
Hizo shirika zina tumika katika shirika za mahali na ina towa msaada wa mapumziko, jamii, na kazi za elimu kwa wana memba wa shirika. Aina moja ya Shirika za jamii ambayo una weza kutana katika shirika lako ni shirika la msingi wa kabila (ECBO). ECBOs zime undwa na wakimbizi wa zamani na wahamaji na zina saidiya wageni katika shirika zao. Zimoja zina towa darasa za elimu kwa watu wazima, zina andaa kundi za wa mama, na kushikilia kazi zaki mila na za mapumziko.
Shirika za imani (FBOs)
Shirika za imani zina jumlisha makanisa, miskiti, masinagogi na mahali zingine za maabudu ambazo lengo yayo niku kuza imani yao. Hata hivyo, kuna piya aina nyingi za sirika za imani, ambazo zina weza pokeya pesa au ku zinaweza ku tiwa kwa mawasiliyana na shirika nyingi za ki dini, ila lengo lao niku towa huduma kwa watu binafsi na jamaa zinazohitaji msaada bila kufwatana na dini yao. Wamoja wanakuwa na darasa za luga ya kingereza kwa watu wazima na wengine wana pana nguo za samani ambazo zimesha tumikishwa.