Mwongozo ya Benye Balifika ba Mupia ya Haki na Usaidizi ya Walemavu nchini Marekani
Huduma mingi zinapatikana kwa watu wenye ulemavu, lakini unaweza kuwa usijue kama au ginsi ya kuzipata na kuzitumia. Unaweza kawa na swali kama:
- Kueleza ulemavu wangu ina weza tatiza hali ya kuama yangu?
- Ni wapi njo naweza pata musahada ya kufikiya uduma?
- Haki zangu ni gani?
- Naweza lomba musahada?
- Kama sasa si ongeye Kingereza muzuri?
- Watu wanaweza elewa mahitaji yangu?
Auko weye peke. Wakimbizi wengi na wapya wenye ulemavu wanakabiliwa na maswali yasawasawa wakishatulia katika jumuiya mpya na kujifunza ginsi mifumo nchini Marekani inavyofanya kazi.
Kuelewa Ulemavu
Ndani ya nchini Marekani, ulemavu unafafanuliwa kisheria kama ulemavu wa kimwili au kiakili ambao inazuia kwa kiasi kikubwa shughuli kubwa moja au zaidi za maisha.
Watu pitiya ulemavu kwa njia tofauti. Ulemavu fulani inaonekana, wakati ingine haionekani.
Kama mtu ikona ulemavu, anaweza kuwa na shida ya kutembea, kusikia, au kuona. Au wanaweza kuishi na maumivu ya muda mrefu, ulemavu wa kujifunza, changamoto za kukumbuka, ulemavu wa maendeleo, hali ya afya ya akili, au matatizo mengine ya afya.
Watu wa moja wana jitambulisha kuwa walemavu. Wengine bado wana weza jifunza ginsi wanavyofikiri kuhusu ulemavu wao au hawatumii neno hilo kwa sababu ya imani zao za kibinafsi, za kitamaduni, au za kidini.
Kujua Haki Zako
Ndani ya nchini Marekani, Sheria ya Wamarekani Wenye Ulemavu (ADA) na sheria zingine nyingi za serikali na shirikisho hulinda watu wenye ulemavu dhidi ya ubaguzi katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na shule, kazi, makazi, usafiri na uduma za afya. Chini ya sheria hii, watu wenye ulemavu wana haki ya kulomba kazi, kuhudhuria shule, na kushiriki katika maisha ya jamii.
Watu wenye ulemavu nchini Marekani wanaweza kustairi kupata usaidizi au makao, bila kujali hali yao ya uhamiaji. Mashirika mingi na huduma za umma lazima zitoe makao ya kueleweka na kufikia kwa watu wenye ulemavu sawasawa. Iyi inaweza kuwa na:
- Huduma za tafsiri
- Kufikiya kiti ya walemavu
- Nyenzo zenye maandishi makubwa
- Muda ya ziada ya kupima au mpangiliyo ya kukutana
- Milango ya kufikiliwa
- Kwa kuingiliya mnyama wa huduma
- Alama za ufikivu wazi katika majengo yote
- Kumbuka: Baadhi ya wenye walifika wapya wenye ulemavu wanaweza pia kustairi kwa makao au kusamehewa wakati wa mchakato wa uraia wa Marekani.
Pia una haki ya kuuliza maswali ikiwa habari haiko wazi wakati wa mupangiliyo ya kukutana au mkutano.
Kuomba Msaada na Makao
Makao ni mabadiliko au usaidizi yaku saidia mtu kushiriki kikamilifu katika maisha ya kila siku. Watu tofauti wanaweza itaji makao tofauti, kama vile viti vinavyonyumbulika, maagizo yaliyoandikwa, chumba tulivu, au mapumziko kutoka kazini kwa mipango ya kukutana ya matibabu.
Kama hujawahi kupata usaidizi unaohusiana na ulemavu hapo zamani au unatoka fasi ambapo ulemavu na afya ya akili haziongelewe waziwazi, unaweza kujisikia wasiwasi kulomba musahada au kuzungumza kuhusu mahitaji yako.
Kulomba musahada ni la kawaida na linakubalika nchini Marekani. Kama ukahitaji kuuliza maswali au kuzungumza ili kupokea makao unayohitaji. Hapa kuna mifano ya kile unacho weza sema:
- "Na tumikisha kiti cha walemavu. Kunaweza kuwa kiingilio enye naweza tumikisha?"
- "Siwezi ona vizuri. Uko na maandishi makubwa sana?"
Waliokuja wapya wengi wana jisikiya muzuri sana kupokea taarifa katika lugha wanayopendelea. Katika hali nyingi, una haki ya kupokea taarifa muhimu katika lugha unayopendelea ya mazungumzo au maandishi. Watoa huduma za afya, shule, na ofisi za serikali zinaweza kutoa watafsiri au huduma za usaidizi wa lugha.
Kama wewe ni Kipofu au ni mgumu wa kusikia, unaweza pia kulomba utafsiri wa lugha ya ishara au usaidizi mwingine wa mawasiliano. Lugha za ishara zina pishana kufatana na inchi. Kama unatumia lugha ya ishara, mwambie mtoa huduma wako lugha ya ishara unayotumia na ginsi unavyo pendelea kuwasiliana.
Kupata Huduma na Msaada
Baadhi ya wenye walifika wapya hawajifunzi kuhusu huduma zinazohusiana na ulemavu na usaidizi apo apo. Kwa sababu hiyo, wanaweza kukosa fursa za kupokea usaidizi unaoweza kurahisisha maisha ya kila siku.
Kulingana na hitaji, msaada unaweza kupatikana juu:
- Huduma ya afya
- Usafiri
- Ajira
- Makazi
- Msaada wa pesa
- Kuishi kwa kujitegemea
Kwa mfano, baadhi ya watu huenda wasijue kama makao au musaada ingine inaweza patikana ikiwa kusafiri kwa mipango ya kukutana au ofisi ni vigumu.
Hata wakati unajua kuwa huduma au ulinzi wa kisheria upo, kutafuta usaidizi na kuelewa ginsi mifumo inavyofanya kazi bado kunaweza kuhisi vigumu au kutokueleweka.
Mipango na mashirika mengi nchini Marekani yanasaidia watu wenye ulemavu. Unaweza kupata musahada kupitia:
- Watoa huduma za makao mupya
- Mashirika ya kijamii
- Mashule
- Wanaotoa huduma za afya
- Mashirika ya kutetea ulemavu
- Jamii ya za imani
- Ofisi za serikali za mitaa
- Mashirika ya musahada wa kisheria
Kama hujui pa kuanzia, muulize mtoa huduma anayeaminika, mfanyakazi wa kesi, au shirika la jumuiya kwa mwongozo. Unaweza pia kutembeleya ADA.gov, Benefits.gov, au saraka ya ILRU Centers for Independent Living ili kupata usaidizi na kutafuta huduma zilizo karibu nawe.
Switchboard imechangia mambo yali omo na ukaguzi wa makala haya.
Vyanzo
- Sheria ya Wamarekani Wenye Ulemavu (ADA): Utangulizi wa Sheria ya Wamarekani Wenye Ulemavu
- Mashirika ya kijamii na rasilimali za utetezi wa walemavu
- Mustafa Rfat: Utafiti na mwongozo wa ulemavu na makao mupya ya wakimbizi
- Huduma za Uraia na Uhamiaji nchini Marekani (USCIS): Makao ya Walemavu kwa Umma
Kanusho: Yaliyomo kwenye tovuti hii yametengenezwa na Settle In, yapo kwenye kikao ya umma, na inaweza kutolewa tena. Nakala iyi inatoa mwongozo yote kuhusu madhumuni ya habari. Sera na desturi mahususi za ulemavu zinaweza kutofautiana kufatana na jimbo na jiji.
IRC ilipokea ufadhili wa kiushindani kupitia Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani, Utawala wa Watoto na Familia, Grant #90RB0053. Mradi iyi inafadhiliwa kwa 100% na pesa za shirikisho. Yaliyomo katika baruwa iyi ni jukumu la waandishi pekee na si lazima yawakilishe maoni rasmi ya Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani, Utawala wa Watoto na Familia.