Elimu

Tengenezeshwa:10/29/2024
Marekani, elimu ina patikana kwa watoto wote, bila kushikamana na uwezo wao, jinsiya, miaka, rangi, dini, mielekezo ya jinsiya, ama nganzi ya kijamii. Pata maelezo zaidi kuhusu Elimu nchini Marekani hapa chini.

Shule za uma ni bure, na kuna kuwa sheriya na kanuni kuhusu elimu ya uma. Elimu ina lazimishwa kwa watoto wa miaka fulani tokeya utoto hadi miaka ya ujana. Miaka kamili kuhusu shurti ya elimu ina pangwa nakila jimbo. Shule zinajingojeya kuona wazazi wana jihusisha na elimu ya watoto wao kwa kuakikisha yakuwa wana fata majifunzo na kuwa saidiya kwa namna mbalimbali.

Image
Education
Image
Education

Watu Wazima

Wa Amerika wanaamini yakuwa mtu hawezi kuwa mzee sana au kijana sana ili kujifunza mambo mapya. Majifunzo ya watu wazima na vijana inawezekana, lakini
wakimbizi wangeli pashwa kwangaliya faida na hasara zaku anza majifunzo kuliko kutafuta kazi. Elimu inaweza kuongoza kwa bahati yaku pata kazi nzuri kwa ujiyo, lakini wakimbizi wanapaswa kutumika punde ili kujibu kwa haja zao wenyewe naza jamaa zao, na majifunzo ya watu wazima Marekani inaweza kuwa ya bei kali. Kwa wakimbizi wengi, chaguo bora inaweza kuwa kutumika muda wote na kwenda shuleni nusu muda.

Jamii nyingi zinatoa aina nyingi za bahati kwa majifunzo ya watu wazima kama vile:

  • Majifunzo ya Kingereza na kujuwa kusoma na kuandika.
  • Majifunzo ya zaidi kwa mambo ya kitekinolojya ya kompyuta, luga za kigeni, na ujuzi za katibu.
  • Developpement d’éducation Générale (GED) kwa watu wazima ambao hawana cheti ya shule ya kisegondari.
  • École Téchnique Vocationnelle.
  • Colège communautaire (kikawaida mipango ya miaka 2).
  • Vyo vikuu ama Yuniversiti (kikawaida mipango ya miaka 4).
  • Vyo vikuu ambazo vina towa vyeti kwa widara nyingi.

Bei ya izo darasa, shule, na vyo vikuu zina pichana zaidi. Shule nyingi na vyo vikuu zina towa msaada wa kipesa kwa wana funzi wanao kuwa nao aja.

Adaptation kwa Réinstallation

Shule za ki Marekani zina kuwa kwa jumla na mazingira ya darasa yaku wasiliyana tafauti na namna ya mafunzo ya hotuba na usemi zinazo tumikishwa kwa inchi zingine. Kunakuwa piya samani inaotolewa kwa wazo nyipya na kazi ya kibinafsi. Kazi za pamoja ni muhimu lakini wana funzi wana pimwa kufatana na kazi wanazo zifanya wenyewe. Wazazi wana eza saidiya watoto wao kwa namna nyingi ata awajuwi vizuri Kingereza.

Ona namna gani muzazi mukimbizi anaweza saidiya kwa elimu ya watoto wao:

  • Ku gunduwa kama shule ina towa matembezi ya elimu ama muelekezo umetolewa kabla masomo ku anza.
  • Uliza mtoto aliyo funjwa siku ile.
  • Uliza mtoto yale anatakiya kufanya nyumbani ama chunguza buku lake la kazi za nyumbani.
  • Uzuriya kwa mafunzo za Kingereza kama lugha ya pili ya masomo, ikiwa wana itowa, kwenye shule ya mtoto wako.
  • Uzuriya kwa mkutano ya wazazi na walimu.
  • Saidiya kwa shuguli zingine za shule kama vile timu ya michezo ya shule, ao kundi ya sanaa.
  • Towa musaada ndani ya darasa ya mtoto wako.
  • Tembeza mtoto wako ndani ya basi ama kwenye shule.
  • Saidiye mtoto wako kwa kazi zake za nyumbani.
Image
Education

Watoto na Vijana

Shule za uma zinapatikana kwa inchi pote bila malipo. Kufatana na sheriya, shule za uma haziwezi kuchukuwa mwelekeyo wa dini fulani. Shule za kibinafsi za patikana eneyo fulani fulani zimoja zinakuwa na mwelekeyo wa kidini. Shule za kibinafsi zinalipisha pesa ya mafunzo, ambayo inaweza kuwa ya bei kali.

Kuna kuwa atuwa ine za elimu kwa watoto Marekani. Watoto wa darasa moja wanaweza kuwa na miaka tafauti, ingawaje watoto wengi wanakuwa na miaka kati ya 1 na 2. Katika shule za uma, vijana wanaume na wabinti wana kuwa wote kwa darasa moja.

Kipusi. Ngazi hiki nikwa watoto toka miaka 3 hadi 5. Ina lazimishwa na sheriya na kawaida sii bure.

Shule ya msingi. Ngazi hii huanza na kipusi (umri wa miaka 5) na ku endelea hadi darasa la tano au la sita (umri wa miaka 12).

Ngazi ya shule ya muelekezo. Ngazi hii kwa kawaida ina jumulisha darasa la sita au la saba hadi darasa la nane au la kenda, kwa watoto wa miaka 12 hadi 14.

Shule ya kisegondari. Ngazi hii kwa kawaida ina jumulisha darasa la kenda au la kumi hadi darasa la kumi na mbili, kwa watoto wa miaka 14 hadi 18. Wanafunzi wanao maliza kwa ngazi hii wana pewa cheti ya kisegondari.

Wanafunzi wanaokuwa na cheti ya shule ya kisegondari alama bora wanaendelesha elimu kwa chuo kikuu, lakini elimu ya juu sii bure. Mafunzo ya kiufundi kisha shule yakisegondari ya patikana pia na ni ya bei rahisi kuliko vyuo vikuu na yuniversiti.

Image
Screenshot of Settle In app
Image
App Icon

Jaza programu ya Settle In

Tazama video fupi, masomo ya kutendana, na beji ya kufuata maendeleo yako ya kujifunza Settle In ndiyo mwenzako msaidizi katika safari yako ya kutafuta makao mupya

Je, makala hii ilikusaidia?
6
0