Kurekebisha Mila

Tengenezeshwa:10/24/2024
Kurekebisha mila ni mwendo unaochukuwa muda mrefu. Mwendo huu ni tafauti kwa watu tofauti, lakini kuna hatua fulani katika huu mwendo ambazo watu wengi wana pitiya kwa Kurekebishwa kwa mila mpya. Pata maelezo zaidi kuhusu Marekebisho ya Kitamaduni nchini Marekani hapa chini.

Marekebisho ya Utamaduni nchini Marekani

Kama unaenda mu Amerike, unaweza kuhisi msisimko na woga. Unapotulia katika maisha yako ya mapya mu nchi ya Amerike, utahisi awamu tofauti za marekebisho.    

Kuna awamu inne za marekebisho ya kitamaduni. Urefu na ukubwa wa kila awamu ni tofauti. Unaweza kupata awamu sawa zaidi ya mara moja au kuruka awamu. 

Awamu ya Honeymoon:  Unahisi kusisimka na furaha kuhusu maisha yako huko Amerike.  

Awamu ya kuharibu kitamaduni: Unajisikia uko na wasiwasi na kuchanganyikiwa unapopitia jumuiya mpya na tofauti. 

Awamu ya Kugewuza: Unajisikia utulivu katika jumuiya yako mpya. Unafurahiya na shughuli za kila siku.     

Awamu kubwa: Unajisikia vizuri na maisha yako mapya na utamaduni. Bado unaweza kuwa na vipindi vigumu, lakini una hisia ya kuwa mali. 

Image
Cultural Adjustment

Unapozoea maisha yako mapya mu nchi ya Amerike, tumia vidokezo hivi zitakusaidia kukabiliana na mfadhaiko na mshtuko wa kitamaduni.  

  • Jifunze Kiingereza itakusaidia kupata kazi, kukutana na watu wapya na kupata marafiki. 
  • Tafuta miunganisho na wengine kwa kwenda kwa matukio ya jumuiya, kucheza michezo au kujitolea. 
  • Fanya mazoezi na ushiriki mila yako ya kitamaduni.  Kwa mfano, kupika chakula kutoka kwa utamaduni wako, kufuata imani za kidini, au kucheza muziki. 
  • Tambua kwamba mienendo ya famille inaweza kugeuka. Kwa mfano, watoto wanaweza kuzoea haraka. Kuwa mvumilivu na wasiliana kwa uwazi na kwa uaminifu na famille yako. 
  • Jifunze baadhi ya kanuni za kijamii za mu Amerike. Kwa mfano, unajua kwamba Wa Amerike wengi wanaamini kuonana ku macho wakati wa mahojiano ya kazi inaonyesha heshima?  
  • Kuwa mvumilivu na mwenye heshima. Mu Inchi ya Amerike, kuna jamii tofauti, mitazamo ya dini, tamaduni, na mielekeo ya ngono.  Ni muhimu kuwaheshimu wengine, hata kama wanatofauti na wewe.  

Ni muhimu kukumbuka kugewuka kwa kitamaduni ni mchakato. Itachukua muda kuzoea maisha katika jumuiya yako mpya. Ikiwa unahitaji usaidizi, uliza Wakala wako wa Makazi Mapya.  

Image
Self sufficiency and self advocacy
Image
Cultural Adjustment
Image
Screenshot of Settle In app
Image
App Icon

Jaza programu ya Settle In

Tazama video fupi, masomo ya kutendana, na beji ya kufuata maendeleo yako ya kujifunza Settle In ndiyo mwenzako msaidizi katika safari yako ya kutafuta makao mupya

Je, makala hii ilikusaidia?
4
0